يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسۡقِي رَبَّهُۥ خَمۡرࣰاۖ وَأَمَّا ٱلۡأٓخَرُ فَيُصۡلَبُ فَتَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِن رَّأۡسِهِۦۚ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ٱلَّذِي فِيهِ تَسۡتَفۡتِيَانِ ٤١
Yusuf 12:41
سورة يوسف
Makka
Aya: 41/111
Ukurasa 240
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watamla kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilo kuwa mkiuliza. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
«Enyi marafiki wangu gerezani, haya uchukueni uaguzi wa ndoto zenu: ama yule aliyeona kwenye ndoto yake kuwa anakamua zabibu, yeye atatoka jela na atakuwa ni mwenye kuishughulikia pombe ya mfalme. Ama mwingine aliyeota kuwa anabeba mkate juu ya kichwa chake, yeye atasulubiwa na aachwe, na ndege waje wamle kichwa chake. Limeshapitishwa jambo ambalo mlikuwa mnaliuliza na limeshamalizwa.»
Yusuf 12:41
Inapakia kisomo…
0:00