وَإِذَا رَأَوۡاْ تِجَٰرَةً أَوۡ لَهۡوًا ٱنفَضُّوٓاْ إِلَيۡهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمٗاۚ قُلۡ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ مِّنَ ٱللَّهۡوِ وَمِنَ ٱلتِّجَٰرَةِۚ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلرَّـٰزِقِينَ
Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na pindi wanapoona baadhi ya Waislamu biashara au chochote miongoni mwa viliwazo vya duniani na pambo lake, hutawanyika kwenda huko na wakakuacha wewe umesimama juu ya mimbari unatoa hutuba. Waambie, ewe Nabii, «Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya thawabu na neema yana manufaa zaidi kwenu kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Bora wa wanaoruzuku na kutoa, basi muombeni na mjisaidie kwa kumtii, ili myapate yaliyoko Kwake ya kheri mbili: ya duniani na ya Akhera.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس