قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ هَادُوٓاْ إِن زَعَمۡتُمۡ أَنَّكُمۡ أَوۡلِيَآءُ لِلَّهِ مِن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, uwaambie wale ambao wameshikamana na desturi za kiyahudi zilizopotoka, «Mkidai kiurongo kwamba nyinyi tu ndio vipenzi vya Mwenyezi Mungu na sio watu wengine, basi tamanini kufa iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu kuwa Mwenyezi Mungu Anawapenda nyinyi.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس