وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na toeni, enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, sehemu ya kile tulichowapa katika njia za kheri, mkilikimbilia hilo kabla ya kifo hakijamjia mmoja wenu na kuziona dalili zake na alama zake, na hapo aseme kwa kujuta, «Mola wangu! Si unipe muda na uahirishe kifo changu kipindi kifupi! Nipate kutoa sadaka sehemu ya mali yangu na niwe miongoni mwa watu wema wachamungu.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس