إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡقَصَصُ ٱلۡحَقُّۚ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٦٢
Al-Imran 3:62
سورة آل عمران
Madina
Aya: 62/200
Ukurasa 58
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu tu, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hakika hili nililokuhadithia, ewe Mtume, kuhusu mambo ya ‘Īsā ndio habari ya kweli isiyo na shaka. Na hakuna muabudiwa anayestahiki ibada isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mshindi katika ufalme Wake, Ndiye Mwenye hekima katika upelekaji mambo Wake na vitendo Vyake.
Al-Imran 3:62
Inapakia kisomo…
0:00