يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقُولُواْ رَٰعِنَا وَقُولُواْ ٱنظُرۡنَا وَٱسۡمَعُواْۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمࣱ ١٠٤
Al-Baqarah 2:104
سورة البقرة
Madina
Aya: 104/286
Ukurasa 16
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Enyi ambao mliamini, msiseme kumwambia Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukie, “Rā’nā.” Yaani: tupatie masikizi yako, utufahamu na utufahamishe. Sababu Mayahudi walikuwa wakisema maneno haya kumwambia Nabii, rehema na amani zimshukie, wakipotoa ndimi zao kwa neno hilo, wakikusudia kumtukana na kumnasibisha na kutoelewa. Na semeni badala yake, enyi Waumini, “Undhurnā.” Yaani: tuangalie na utuchunge. Lina maana yale-yale yanayokusudiwa. «Na msikie Kitabu cha Mola wenu mnachosomewa na mkifahamu.» Na wenye kukanusha wana adhabu yenye kuumiza.
Al-Baqarah 2:104
Inapakia kisomo…
0:00