وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ لَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةࣰ فَنَتَبَرَّأَ مِنۡهُمۡ كَمَا تَبَرَّءُواْ مِنَّاۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ ٱللَّهُ أَعۡمَٰلَهُمۡ حَسَرَٰتٍ عَلَيۡهِمۡۖ وَمَا هُم بِخَٰرِجِينَ مِنَ ٱلنَّارِ ١٦٧
Al-Baqarah 2:167
سورة البقرة
Madina
Aya: 167/286
Ukurasa 25
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na wale wafuasi watasema, «Twatamani tuwe na marejeo ya duniani, ili tutangaze kujitenga kwetu na hawa viongozi kama walivyotangaza kujitenga kwao na sisi.» Na kama Alivyowaonesha Mwenyezi Mungu ukali wa adhabu Yake, Siku ya Kiyama, Atawaonesha vitendo vyao viovu kuwa ni majuto kwao. Na hawatakuwa ni wenye kutoka Motoni kabisa.
Al-Baqarah 2:167
Inapakia kisomo…
0:00