فَمَنۡ خَافَ مِن مُّوصࣲ جَنَفًا أَوۡ إِثۡمࣰا فَأَصۡلَحَ بَيۡنَهُمۡ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورࣱ رَّحِيمࣱ ١٨٢
Al-Baqarah 2:182
سورة البقرة
Madina
Aya: 182/286
Ukurasa 28
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na mwenye kumkhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Basi yoyote atakayejua kuwa mwenye kuusia amepinduka, kwa kuiacha haki katika wasia wake kwa njia ya kukosea au kukusudia, akamnasihi mtoaji wasia, wakati wa kutoa wasia, afanye uadilifu, na iwapo hilo halikuwa akaleta upatanishi kati ya pande zinazohusika kwa kugeuza wasia ili ulingane na Sheria, basi atakuwa hana dhambi katika kupatanisha huku. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye huruma kwao.
Al-Baqarah 2:182
Inapakia kisomo…
0:00