زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَيَسۡخَرُونَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۘ وَٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَٱللَّهُ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابࣲ ٢١٢
Al-Baqarah 2:212
سورة البقرة
Madina
Aya: 212/286
Ukurasa 33
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Walio kufuru wamepambiwa maisha ya duniani; na wanawafanyia maskhara walio amini. Na wenye kuchamngu watakuwa juu yao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wale walioukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu wamepambiwa maisha ya dunia na vilivyomo humo vya matamanio na vilivyo tamu, na huku wao wanawafanyia shere Waumini. Na hawa wanaomcha Mola wao watakuwa juu ya Makafiri wote Siku ya Kiyama, ambapo Mwenyezi Mungu Atawatia katika Pepo ya daraja za juu na Atawateramsha Makafiri ndani ya mashimo ya Moto ya chini. Mwenyezi Mungu Anamruzuku Amtakaye, katika viumbe vyake, bila ya hesabu.
Al-Baqarah 2:212
Inapakia kisomo…
0:00