وَلَا تُؤۡتُواْ ٱلسُّفَهَآءَ أَمۡوَٰلَكُمُ ٱلَّتِي جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ قِيَٰمࣰا وَٱرۡزُقُوهُمۡ فِيهَا وَٱكۡسُوهُمۡ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلࣰا مَّعۡرُوفࣰا ٥
An-Nisa' 4:5
سورة النساء
Madina
Aya: 5/176
Ukurasa 77
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu. Walisheni katika hayo na muwavike, na mseme nao maneno mazuri. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wala msiwape, enyi wasimamizi, wale wafujaji, kati ya wanaume, wanawake na watoto, mali zao ambazo ziko chini ya mikono yenu, kwani wataziweka sehemu isiyokuwa yake. Mali hizi ndizo ambazo juu yake yanasimama maisha ya watu. Wapeni matumizi na mavazi, kwenye mali hizo, na muwaambie maneno mazuri yanayopendeza na muamiliane nao kwa tabia njema.
An-Nisa' 4:5
Inapakia kisomo…
0:00