إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمۡۗ وَتَمَّتۡ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ ١١٩
Hood 11:119
سورة هود
Makka
Aya: 119/123
Ukurasa 235
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Isipokuwa wale waliorehemewa na Mola wako, wakamuamini Yeye na wakawafuata Mitume Wake, kwani wao hawatafautiani juu ya kumpwkwesha Mwenyezi Mungu na yale ambayo Mitume wamekuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni matakwa ya Hekima Yake, Aliyetakata na sifa za upungufu na Akatukuka, kwamba Yeye Amewaumba wao wakiwa wametafautiana: kuna kundi ovu na kundi lema; na kila kundi limesahilishiwa kwa lile lililoumbiwa, na kwa hii ndipo agizo la Mwenyezi Mungu litatimia la kuwa Yeye Ataujaza, Moto wa Jahanamu, majini na binadamu waliomfuata Iblisi na askari wake na wasiongoke kwenye njia ya Imani.
Hood 11:119
Inapakia kisomo…
0:00