قُل لَّوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوۡتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَدۡرَىٰكُم بِهِۦۖ فَقَدۡ لَبِثۡتُ فِيكُمۡ عُمُرࣰا مِّن قَبۡلِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ١٦
Yunus 10:16
سورة يونس
Makka
Aya: 16/109
Ukurasa 210
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni. Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii? -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Waambie, ewe Mtume, «Lau Mwenyezi Mungu Alitaka, singaliwasomea hii Qur’ani, wala Mwenyezi Mungu Hangaliwajulisha nayo. Basi jueni kuwa hiyo ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Kwani nyinyi mnajua kwamba mimi nimekaa na nyinyi muda mrefu kabla Mola wangu Hajauleta wahyi wa hiyo (Qur’ani) kwangu, na kabla sijaisoma kwenu. Basi hamtumii akili zenu kwa kuzingatia na kufikiri?»
Yunus 10:16
Inapakia kisomo…
0:00