قَالَتۡ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِي لُمۡتُنَّنِي فِيهِۖ وَلَقَدۡ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ فَٱسۡتَعۡصَمَۖ وَلَئِن لَّمۡ يَفۡعَلۡ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسۡجَنَنَّ وَلَيَكُونࣰا مِّنَ ٱلصَّٰغِرِينَ ٣٢
Yusuf 12:32
سورة يوسف
Makka
Aya: 32/111
Ukurasa 239
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Yule bibi aksema: Huyu basi ndiye huyo mliye nilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na akitofanya ninayo muamrisha basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio chini kabisa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Mke wa kiongozi alisema kuwaambia wanawake waliojikata mikono yao, «Haya ndiyo yaliyowapata kwa kumuona yeye. Aliyefanya mpatikane na haya ni huyu kijana ambaye nyinyi mumenilaumu kusalitika naye. Kwa kweli nilimtaka na nikajaribu kumvutia ili anikubalie, akajizuia na akakataa. Na asipofanya ninachomuamuru mbeleni, atateswa kwa kutiwa jela na hapo atakuwa ni miongoni mwa wanyonge.
Yusuf 12:32
Inapakia kisomo…
0:00