قَالَ لَا يَأۡتِيكُمَا طَعَامࣱ تُرۡزَقَانِهِۦٓ إِلَّا نَبَّأۡتُكُمَا بِتَأۡوِيلِهِۦ قَبۡلَ أَن يَأۡتِيَكُمَاۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّيٓۚ إِنِّي تَرَكۡتُ مِلَّةَ قَوۡمࣲ لَّا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ ٣٧
Yusuf 12:37
سورة يوسف
Makka
Aya: 37/111
Ukurasa 239
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Akasema: Hakitakufikilieni chakula mtakacho pewa ila nitakwambieni hakika yake kabla hakijakufikieni. Haya ni katika yale aliyo nifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasio muamini Mwenyezi Mungu, na wakawa hawaiamini Akhera. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Yūsuf aliwaambia, «Hamtajiwa na riziki ya chakula kwa namna yoyote ile, isipokuwa mimi nitawapa tafsiri yake kabla ya kuwajia. Tafsiri hiyo nitakayowapa nyinyi wawili ni miongoni mwa yale niliyofundishwa na Mola wangu. Mimi nimemuamini na nimemtakasia ibada na nimejiepusha na dini ya wasiomuamini Mwenyezi Mungu wala kuamini kufufuliwa na kuhesabiwa.
Yusuf 12:37
Inapakia kisomo…
0:00