إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ كُبِتُواْ كَمَا كُبِتَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَقَدۡ أَنزَلۡنَآ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Hakika wanao pinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale walio kuwa kabla yao. Na tulikwisha teremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika ya wale wanaomfanyia uadui na Mwenyezi mungu na Mtume Wake na wakaenda kinyume na amri zao, watadhalilishwa na watatwezwa kama walivyodhalilishwa ummah waliokuwa kabla yao waliopingana na Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. Na tumeteremsha aya zenye hoja zilizo wazi zinazoonyesha kuwa Sheria ya Mwenyezi Mungu na mipaka Yake ni kweli. Na wenye kuzikanusha aya hizo watapata adhabu yenye kudhalilisha ndani ya moto wa Jahanamu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس