يَوۡمَ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓاْۚ أَحۡصَىٰهُ ٱللَّهُ وَنَسُوهُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Siku atapo wafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyo yatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kumbuka, ewe Mtume, Siku ya Kiyama, Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atawahuisha wafu wote na Atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho katika uwanja mmoja, Awape habari ya yale waliyoyafanya ya kheri na shari. Mwenyezi Mungu Ameyadhibiti hayo na Ameyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa, na Amewatunzia wao katika kurasa za matendo yao na hali wao wameyasahau. Na Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila jambo, hakuna chochote kinachofichamana Kwake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس