وَقَرۡنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجۡنَ تَبَرُّجَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ ٱلۡأُولَىٰۖ وَأَقِمۡنَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتِينَ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِعۡنَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُذۡهِبَ عَنكُمُ ٱلرِّجۡسَ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِ وَيُطَهِّرَكُمۡ تَطۡهِيرࣰا ٣٣
AlAhzab 33:33
سورة الأحزاب
Madina
Aya: 33/73
Ukurasa 422
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Najilazimisheni kuwa majumbani mwenu, na msitoke humo isipokuwa kwa mahitaji, na msionyeshe uzuri wenu kama vile wanawake wa kipindi cha ujinga wa mwanzo walivyokuwa wakifanya, katika zama zilizotangulia Uislamu. Na maneno haya wanaambiwa wanawake wa kila zama. Na tekelezeni, enyi wake wa Nabii, Swala kwa ukamilifu katika nyakati zake, na toeni Zaka kama Alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika maamrisho yao na makatazo yao. Hakika si lingine Mwenyezi Mungu Amewausia haya ili Awasafishe nyinyi na Awaondolee udhia na ubaya enyi watu wa nyumba ya Nabii!, ambao miongoni mwao ni wake zake na wanaozalikana na yeye, rehema na amani zimshukie, na Azitakase nafsi zenu upeo wa kuzitakasa.
AlAhzab 33:33
Inapakia kisomo…
0:00