وَٱلَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِن نِّسَآئِهِمۡ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُواْ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مِّن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۚ ذَٰلِكُمۡ تُوعَظُونَ بِهِۦۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wale wanaojiharamishia wake zao kwa kuwafananisha na migongo ya mama zao kisha wakarudi nyuma na hilo neno na wakataka kuwaingilia, basi ni juu ya yule mume aliyetoa tamshi la ẓihār, katika hali hii, atoe kafara ya kule kujiharamishia, nayo ni kuacha shingo huru yenye Imani: mtumwa au kijakazi, kabla hajamuingilia yule mkewe aliyemfananisha na mgongo wa mamake. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa anayemfananisha mkewe na mgongo wa mamake, mnakumbushwa mwaidhike nayo, enyi Waumini, ili msiingie kwenye kosa la kuwafananisha wake zenu na mama zenu na kusema neno la uzushi, na mtoe kafara mnapoingia kwenye kosa hilo, na ili msirudie tena kufanya hilo. Na Mwenyezi Mungu hakifichamani chochote Kwake Yeye katika matendo yenu, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwayo
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس