مَثَلُ ٱلَّذِينَ حُمِّلُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ ثُمَّ لَمۡ يَحۡمِلُوهَا كَمَثَلِ ٱلۡحِمَارِ يَحۡمِلُ أَسۡفَارَۢاۚ بِئۡسَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mfano wa Mayahudi ambao walitakiwa kuifuata Taurati kivitendo kisha wakakosa kuifuata ni kama mfano wa punda ambaye yuwabeba vitabu na hajui yaliyo ndani yake. Ni mfano muovu mno wa watu ambao wamezikataa aya za Mwenyezi Mungu na wasifaidike nazo. Na Mwenyezi mungu Hawaelekezi kwenye wema watu madhalimu ambao wanaikiuka mipaka Yake na wanaotoka nje ya utiifu Kwake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس