Sura Ad-Dukhan kwa Kiswahili
سورة الدخان · Aya: 59 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
حمٓ
Ad-Dukhan
H'a Mim -
2
وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha, -
3
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةࣲ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. -
4
فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima, -
5
أَمۡرࣰا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ
Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. -
6
رَحۡمَةࣰ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. -
7
رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. -
8
لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. -
9
بَلۡ هُمۡ فِي شَكࣲّ يَلۡعَبُونَ
Lakini wao wanacheza katika shaka. -
10
فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانࣲ مُّبِينࣲ
Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, -
11
يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمࣱ
Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu! -
12
رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ
Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. -
13
أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولࣱ مُّبِينࣱ
Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. -
14
ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمࣱ مَّجۡنُونٌ
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. -
15
إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ
Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! -
16
يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. -
17
۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولࣱ كَرِيمٌ
Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. -
18
أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينࣱ
Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. -
19
وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِۖ إِنِّيٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَٰنࣲ مُّبِينࣲ
Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. -
20
وَإِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمۡ أَن تَرۡجُمُونِ
Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. -
21
وَإِن لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ لِي فَٱعۡتَزِلُونِ
Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. -
22
فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَٰٓؤُلَآءِ قَوۡمࣱ مُّجۡرِمُونَ
Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu. -
23
فَأَسۡرِ بِعِبَادِي لَيۡلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. -
24
وَٱتۡرُكِ ٱلۡبَحۡرَ رَهۡوًاۖ إِنَّهُمۡ جُندࣱ مُّغۡرَقُونَ
Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa. -
25
كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّٰتࣲ وَعُيُونࣲ
Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! -
26
وَزُرُوعࣲ وَمَقَامࣲ كَرِيمࣲ
Na mimea na vyeo vitukufu! -
27
وَنَعۡمَةࣲ كَانُواْ فِيهَا فَٰكِهِينَ
Na neema walizo kuwa wakijistareheshea! -
28
كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ
Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. -
29
فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ
La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. -
30
وَلَقَدۡ نَجَّيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ
Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, -
31
مِن فِرۡعَوۡنَۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيࣰا مِّنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. -
32
وَلَقَدِ ٱخۡتَرۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ عِلۡمٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. -
33
وَءَاتَيۡنَٰهُم مِّنَ ٱلۡأٓيَٰتِ مَا فِيهِ بَلَٰٓؤࣱاْ مُّبِينٌ
Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi. -
34
إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ
Hakika hawa wanasema: -
35
إِنۡ هِيَ إِلَّا مَوۡتَتُنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُنشَرِينَ
Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. -
36
فَأۡتُواْ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. -
37
أَهُمۡ خَيۡرٌ أَمۡ قَوۡمُ تُبَّعࣲ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. -
38
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. -
39
مَا خَلَقۡنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. -
40
إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ مِيقَٰتُهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote. -
41
يَوۡمَ لَا يُغۡنِي مَوۡلًى عَن مَّوۡلࣰى شَيۡـࣰٔا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. -
42
إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. -
43
إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ
Hakika Mti wa Zaqqum, -
44
طَعَامُ ٱلۡأَثِيمِ
Ni chakula cha mwenye dhambi. -
45
كَٱلۡمُهۡلِ يَغۡلِي فِي ٱلۡبُطُونِ
Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni -
46
كَغَلۡيِ ٱلۡحَمِيمِ
Kama kutokota kwa maji ya moto. -
47
خُذُوهُ فَٱعۡتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ
(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! -
48
ثُمَّ صُبُّواْ فَوۡقَ رَأۡسِهِۦ مِنۡ عَذَابِ ٱلۡحَمِيمِ
Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka. -
49
ذُقۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡكَرِيمُ
Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! -
50
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمۡتَرُونَ
Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka. -
51
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينࣲ
Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani, -
52
فِي جَنَّٰتࣲ وَعُيُونࣲ
Katika mabustani na chemchem, -
53
يَلۡبَسُونَ مِن سُندُسࣲ وَإِسۡتَبۡرَقࣲ مُّتَقَٰبِلِينَ
Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana, -
54
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينࣲ
Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini. -
55
يَدۡعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ
Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. -
56
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلۡمَوۡتَ إِلَّا ٱلۡمَوۡتَةَ ٱلۡأُولَىٰۖ وَوَقَىٰهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ
Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu, -
57
فَضۡلࣰا مِّن رَّبِّكَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. -
58
فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. -
59
فَٱرۡتَقِبۡ إِنَّهُم مُّرۡتَقِبُونَ
Ngoja tu, na wao wangoje pia.