Sura An-Nas kwa Kiswahili
سورة الناس · Aya: 6 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ
An-Nas
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, -
2
مَلِكِ ٱلنَّاسِ
Mfalme wa wanaadamu, -
3
إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ
Mungu wa wanaadamu, -
4
مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ
Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, -
5
ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ
Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, -
6
مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ
Kutokana na majini na wanaadamu.