أَفَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ فَرَءَاهُ حَسَنٗاۖ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۖ فَلَا تَذۡهَبۡ نَفۡسُكَ عَلَيۡهِمۡ حَسَرَٰتٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ
Je! Yule aliye pambiwa a'mali zake mbaya na akaziona ni njema - basi hakika Mwenyezi Mungu humwacha akapotea amtakaye, na humwongoa amtakaye. Basi nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anajua wanayo yafanya.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Je, yule ambaye Shetani anampambia matendo yake maovu ya kumuasi Mwenyezi Mungu, kukufuru na kuwaabudu wasiyekuwa Yeye miongoni mwa waungu na masanamu, akayaona ni mazuri yenye kupendeza, (Je, yeye) ni kama yule ambaye Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amemuongoza akaliona zuri kuwa ni zuri na ovu kuwa ni ovu? Hakika Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayemtaka na Anamuongoza Anayemtaka. Basi usijiangamize kwa kuwa na huzuni juu ya ukanushaji wa hawa waliopotea. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua maovu yao na Atawalipa kwa hayo malipo mabaya kabisa.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس