ترجمة سورة الماعون

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ترجمة معاني سورة الماعون باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس .

Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa?
Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake.
Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?.
Basi adhabu kali itawafikia wenye kusali,
ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake.
Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria.
Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kumuabudu Mola wao wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake.
Icon