يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَيۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَٰمُ رِجۡسٞ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo! Hakika pombe: nayo ni kila kinacholewesha kinachofinika akili, al-maysir, nayo ni kamari ambayo inakusanya aina za kuwekeana dau na mfano wake, kama zile za kuekeana badali kutoka pande mbili za wacheza kamari na kuzuia kumtaja Mwenyezi Mungu, al-ansab: mawe ambayo washirikina walikuwa wakichinja mbele yake kwa njia ya kuyatukuza na yale yanayosimamishwa ili kujisongeza karibu yake kwa ibada na al-azlam: vipande vinavyotumiwa na makafiri kutafuta uamuzi kabla ya kufanya au kuacha kufanya jambo. Hayo yote ni dhambi inayopambiwa na Shetani. Basi jiepusheni na madhambi haya, huenda nyinyi mkafuzu kwa kupata Pepo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس