Sura Al-Ma'arij kwa Kiswahili
سورة المعارج · Aya: 44 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابࣲ وَاقِعࣲ
Al-Ma'arij
Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, -
2
لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعࣱ
Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - -
3
مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ
Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. -
4
تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمࣲ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةࣲ
Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! -
5
فَٱصۡبِرۡ صَبۡرࣰا جَمِيلًا
Basi subiri kwa subira njema. -
6
إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدࣰا
Hakika wao wanaiona iko mbali, -
7
وَنَرَىٰهُ قَرِيبࣰا
Na Sisi tunaiona iko karibu. -
8
يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ
Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. -
9
وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ
Na milima itakuwa kama sufi. -
10
وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمࣰا
Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. -
11
يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ
Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, -
12
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ
Na mkewe, na nduguye, -
13
وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ
Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, -
14
وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعࣰا ثُمَّ يُنجِيهِ
Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. -
15
كَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ
La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, -
16
نَزَّاعَةࣰ لِّلشَّوَىٰ
Unao babua ngozi ya kichwa! -
17
تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ
Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. -
18
وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ
Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. -
19
۞ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا
Hakika mtu ameumbwa na papara. -
20
إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعࣰا
Inapo mgusa shari hupapatika. -
21
وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا
Na inapo mgusa kheri huizuilia. -
22
إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ
Isipo kuwa wanao sali, -
23
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ
Ambao wanadumisha Sala zao, -
24
وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقࣱّ مَّعۡلُومࣱ
Na ambao katika mali yao iko haki maalumu -
25
لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; -
26
وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, -
27
وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ
Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. -
28
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونࣲ
Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. -
29
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ
Na ambao wanahifadhi tupu zao. -
30
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ
Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - -
31
فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ
Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. -
32
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, -
33
وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ
Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, -
34
وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ
Na ambao wanazihifadhi Sala zao. -
35
أُوْلَٰٓئِكَ فِي جَنَّٰتࣲ مُّكۡرَمُونَ
Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. -
36
فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ
Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? -
37
عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ
Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! -
38
أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيࣲٕ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمࣲ
Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? -
39
كَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ
La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. -
40
فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza -
41
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيۡرࣰا مِّنۡهُمۡ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. -
42
فَذَرۡهُمۡ يَخُوضُواْ وَيَلۡعَبُواْ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ
Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, -
43
يَوۡمَ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ سِرَاعࣰا كَأَنَّهُمۡ إِلَىٰ نُصُبࣲ يُوفِضُونَ
Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, -
44
خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةࣱۚ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلَّذِي كَانُواْ يُوعَدُونَ
Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa.