أَفَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلۡمٖ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمۡعِهِۦ وَقَلۡبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَٰوَةٗ فَمَن يَهۡدِيهِ مِنۢ بَعۡدِ ٱللَّهِۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Unamuona vipi, ewe Mtume, yule aliyoyachukuwa matamanio yake akayafanya ndiye Mola wake, akawa hatamani kitu isipokuwa anakifanya, na Mwenyezi Mungu Akampoteza baada ya ujuzi kumfikia na kusimamiwa na hoja, akawa hasikii mawaidha ya Mwenyezi Mungu wala hazingatii kwa mawaidha hayo, na Mwenyezi Mungu akapiga muhuri juu ya moyo wake akawa hafahamu kitu, na Akaweka finiko kwenye macho yake akawa hazioni hoja za Mwenyezi Mungu? Basi ni nani atakayemuongoza kuifikia haki na uongofu baada ya Mwenyezi Mungu kumpoteza? Kwani hamkumbuki, enyi watu mkajua kwamba mwenye kufanywa hivyo na Mwenyezi Mungu hataongoka kabisa na hatapata wa kumsaidia na kumuongoza? Aya hii ndio msingi wa kuonya kwamba matamanio hayafai kuwa ndio msukumo wa Waumini katika matendo yao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس