بَلۡ ظَنَنتُمۡ أَن لَّن يَنقَلِبَ ٱلرَّسُولُ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ إِلَىٰٓ أَهۡلِيهِمۡ أَبَدٗا وَزُيِّنَ ذَٰلِكَ فِي قُلُوبِكُمۡ وَظَنَنتُمۡ ظَنَّ ٱلسَّوۡءِ وَكُنتُمۡ قَوۡمَۢا بُورٗا
Lakini mlidhani kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana mbaya, na mkawa watu wanao angamia.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Pia mambo sivyo kama mlivyodai kuwa mlishughulishwa na mali na watu wa nyumbani, bali kwa kweli nyinyi mlidhani kuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wale Maswahaba waliokuwa na yeye wataangamia na hawatarudi kwenu kabisa, na Shetani aliwapambia hilo ndani ya nyoyo zenu. Na pia mlidhani dhana mbaya kuwa Mwenyezi Mungu Hatampa ushindi Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Maswahaba wake juu ya maadui wao, na mlikuwa ni watu wenye kuangamia msiokuwa na kheri yoyote.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس