وَأُخۡرَىٰ لَمۡ تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهَا قَدۡ أَحَاطَ ٱللَّهُ بِهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٗا
Na mengine hamwezi kuyapata bado, Mwenyezi Mungu amekwisha yazingia. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hakika Mwenyezi Mungu Amewaahidi nyinyi ngawira nyingine ambayo hamna uwezo nayo, Mwenyezi Mungu, kutakasika na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mwenye uweza nayo, nayo iko chini ya mpango Wake na mamlaka Yake, na Ashawaahidi nyinyi kuwapatia, na hapana budi kwamba kile Alichoahidi kitakuwa. Na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna chochote kinachomshinda.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس