قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ ٱللَّهُمَّ رَبَّنَآ أَنزِلۡ عَلَيۡنَا مَآئِدَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ تَكُونُ لَنَا عِيدٗا لِّأَوَّلِنَا وَءَاخِرِنَا وَءَايَةٗ مِّنكَۖ وَٱرۡزُقۡنَا وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلرَّـٰزِقِينَ
Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
‘Īsā mwana wa Maryam Aliyakubali matakwa ya Ḥawāriyyūn akamuomba Mola wake , Aliyetukuka na kuwa juu, kwa kusema, «Mola wetu! Tuteremshie meza ya chakula kutoka mbinguni, tupate kuifanya siku hiyo ya kuteremka kwake ni sikukuu kwetu, sisi tutaitukuza na pia watakaokuja baada yetu, na hiyo meza itakuwa ni alama na ni hoja kutoka kwako , ewe Mwenyezi Mungu, juu ya upweke wako na juu ya ukweli wa unabii wangu, na ututunuku miongoni mwa vipewa vyako vyingi, na wewe ndiye bora wa wenye kuruzuku.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس