إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِن قَبۡلِ أَن تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهِمۡۖ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Isipo kuwa wale walio tubu kabla hamjawatia nguvuni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Lakini atakayekuja kati ya wale wanaopiga vita kabla hamjawatia mkononi na akaja akiwa mtiifu mwenye majuto, atafutiwa yale yaliyokuwa ni haki ya Mwenyezi Mungu. Na jueni, enyi Waumini, kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye kuwarehemu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس