وَكَيۡفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ ٱلتَّوۡرَىٰةُ فِيهَا حُكۡمُ ٱللَّهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوۡنَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَـٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si wenye kuamini.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kitendo cha Mayahudi hawa ni cha kushangaza. Wao wanashitakiana kwako, ewe Mtume, na wao hawakuamini wewe wala Kitabu chako, pamoja na kuwa ile Taurati wanayoiamini wanayo, na humo muna hukumu ya Mwenyezi Mungu; kisha wanaondoka baada ya kutoa hukumu yako, iwapo haikuwaridhisha, wakakusanya kati ya kuzikataa sheria zao na kuipa mgongo hukumu yako. Na hawakuwa hao, wanaosifika na sifa hizo, ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu, kukuamini wewe na kuikubali hukumu uliyoitoa.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس