وَتَرَىٰ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَأَكۡلِهِمُ ٱلسُّحۡتَۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi, na uadui, na ulaji wao vya haramu. Ni maovu mno hayo wayatendayo!
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na utawaona, ewe Mtume, wengi miongoni mwa Mayahudi wanayakimbilia maasia ya kusema urongo, uzushi, kuzifanyia uadui hukumu za Mwenyezi Mungu na kula mali ya watu kinyume na haki. Ni maovu mno matendo yao na uadui wao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس