أُحِلَّ لَكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَحۡرِ وَطَعَامُهُۥ مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِلسَّيَّارَةِۖ وَحُرِّمَ عَلَيۡكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَرِّ مَا دُمۡتُمۡ حُرُمٗاۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ
Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini na kuvila, kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya wanyama wa bara maadamu mmeharimia Hija. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mwenyezi Mungu Amewahalalishia, enyi Waislamu, mtapokuwa kwenye hali ya ihramu, viwindwa wa baharini, nao niwale wavuliwao baharini wakiwa hai, na chakula chake, nacho ni kiumbe kilichokufa kitokacho humo, kwa ajili mnufaike mkiwa ni wakazi au ni wasafiri. Na Ameharamishia viwindwa wa barani muko kwenye ihramu ya Hija au ya Umra. Na muogopeni Mwenyezi Mungu na mtekeleze amri Zake zote na mjiepushe na makatazo Yake yote, mpaka mfuzu kwa thawabu Zake kubwa na msalimike na ukali wa mateso Yake mnapofufuliwa ili mhesabiwe na mlipwe.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس