قَالُواْ رَبَّنَآ أَمَتَّنَا ٱثۡنَتَيۡنِ وَأَحۡيَيۡتَنَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَٱعۡتَرَفۡنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلۡ إِلَىٰ خُرُوجٖ مِّن سَبِيلٖ
Watasema: Mola wetu Mlezi! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Makafiri watasema, «Mola wetu! Umetufisha mara mbili: tulipokuwa matone ya manii ndani ya matumbo ya mama zetu kabla ya kupulizwa roho na ulipokoma muda wetu wa kuishi katika uhai wa duniani, na umetuhuisha mara mbili:katika nyumba ya duniani siku tuliyozaliwa na siku tuliyofufuliwa kutoka makaburini mwetu. Kwa hivyo sisi sasa tunakubali makosa yetu yaliyotangulia, basi je kuna njia yoyote ya sisi kutoka Motoni na uturudishe kupitia njia hiyo duniani tukapate kufanya matendo ya utiifu kwako?» Lakini haliwi hilo kabisa la wao kunufaika kwa kukubali kwao huku.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس