فَسَتَذۡكُرُونَ مَآ أَقُولُ لَكُمۡۚ وَأُفَوِّضُ أَمۡرِيٓ إِلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ
Basi mtayakumbuka ninayo kuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona waja wake.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Alipowasihi na wasimkubalie aliwaambia, «Basi mtakumbuka kuwa mimi niliwasihi na nikawakumbusha, na mtajuta wakati ambao majuto hayatanufaisha. Na mimi ninahamia kwa Mola wangu nataka hifadhi Yake na ninamtegemea Yeye, hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, ni Mtambuzi wa hali za waja na malipo wanayostahiki malipo, hakuna kinachofichamana Kwake chochote katika hayo.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس