ٱلَّذِينَ يَحۡمِلُونَ ٱلۡعَرۡشَ وَمَنۡ حَوۡلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْۖ رَبَّنَا وَسِعۡتَ كُلَّ شَيۡءٖ رَّحۡمَةٗ وَعِلۡمٗا فَٱغۡفِرۡ لِلَّذِينَ تَابُواْ وَٱتَّبَعُواْ سَبِيلَكَ وَقِهِمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ
Wale wanao beba A'rshi, na wanao izunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wale wanaoibeba ‘Arshi ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa Malaika na wale walioko pambizoni mwake kati ya wale wanaoizunguka miongoni mwao, wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kasoro, wanamshukuru kwa yale Anayostahiki, wanamuamini Yeye haki ya kumuamini na wanamuomba Awasamehe Waumini kwa kusema, «Mola wetu! Umekienea kile kitu kwa rehema na ujuzi. Kwa hivyo wasamehe wale waliotubia kutokana na ushirikina na maasia na wakafuata njia uliyowaamrisha waifuate, nayo ni Uislamu, na uwaepushie adhabu ya Moto na vituko vyake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس