ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِٱلشَّهَٰدَةِ عَلَىٰ وَجۡهِهَآ أَوۡ يَخَافُوٓاْ أَن تُرَدَّ أَيۡمَٰنُۢ بَعۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡمَعُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Hivi inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi ulio sawa au wataogopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao. Na mcheni Mwenyezi Mungu na msikie. Na hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi wapotofu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hukumu hiyo ya kuapa baada ya Swala na kutokubali ushahidi wa hao wawili, baada ya kuutilia shaka, ndiyo inayouleta karibu zaidi uwezekano wa wao kutoa ushahidi kama ulivyo kwa kuogopa adhabu ya Akhera au kwa kuchelea yamini lao la urongo lisikataliwe na wale wenye haki baada ya kuapa kwao na asije akafedheheka yule mrongo ambaye yamini lake lilikakataliwa hapa ulimwenguni baada ya kufunuka uhaini wake. Na muogopeni Mwenyezi Mungu, enyi watu, na mumtunze msije mukaapa kiapo cha urongo na msije mkanyakuwa kwa mayamini yenu mali ya haramu. Na msikie mnayowaidhiwa nayo. Na Mwenyezi Mungu Hawaongozi watu wenye nyendo mbaya waliotoka nje ya utiifu Wake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس