يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱبۡتَغُوٓاْ إِلَيۡهِ ٱلۡوَسِيلَةَ وَجَٰهِدُواْ فِي سَبِيلِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Yake kivitendo, muogopeni Mwenyezi Mungu na mjisogeze karibu Kwake kwa kumtii na kufanya yanayomridhisha, na mpigane jihadi katika njia Yake ili mpate kufaulu kwa kuingia mabustani ya Pepo Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس