قُلۡ هَلۡ أُنَبِّئُكُم بِشَرّٖ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيۡهِ وَجَعَلَ مِنۡهُمُ ٱلۡقِرَدَةَ وَٱلۡخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَۚ أُوْلَـٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ
Sema: Je! Nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet'ani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wamepotea zaidi njia iliyo sawa.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Nabii, kuwaambia Waumini, «Je, niwajulishe yule ambaye atalipwa, Siku ya Kiyama, malipo makali zaidi kuliko hawa wenye kutoka nje ya utiifu?» Hao ni waliowatangulia wao ambao Mwenyezi Mungu Aliwafukuza kwenye rehema Yake, Aliwakasirikia na akawageuza maumbile yao Akawafanya manyani na ngurue kwa kuasi kwao, kuzua kwao urongo na kuwa na kiburi, kama ambavyo walikuwa kati yao wenye kuabudu Tāghūt (kila kinachoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu nacho kimeridhika). Hao, ni pabaya mno mahali pao huko Akhera; na harakati zao ulimwenguni zilikosa mwelekeo wa njia ya sawa.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس