لَقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمۡۖ إِنَّهُۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَىٰهُ ٱلنَّارُۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ
Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaapa kwamba wale ambao walisema, «Mwenyezi Mungu Ndiye al-Masīh, mwana wa Maryam,» wameshakufuru kwa maneno yao haya. Na Alitoa habari Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwamba al- Masīh, alisema kuwaambia Wana wa Isrāīl, «Muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika, kwani mimi na nyinyi katika uja tuko sawa.» Kwa hakika, yoyote atakayemuabudu mwengine, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliye Pweke, basi Mwenyezi Mungu Ataifanya Pepo kuwa ni haramu kwake na Ataufanya Moto kuwa ndio makao yake na hatakuwa na msaidizi wa kumuokoa nao Moto huo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس