قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ تَكُ تَأۡتِيكُمۡ رُسُلُكُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ قَالُواْ بَلَىٰۚ قَالُواْ فَٱدۡعُواْۗ وَمَا دُعَـٰٓؤُاْ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٍ
Nao watasema: Je! Hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilio wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Washika hazina wa Jahanamu waseme kuwaambia kwa njia ya kuwakaripia na kuwalaumu, «Maombi haya hayatafalia kitu. Kwani hawakuwajia nyinyi Mitume wenu na hoja waziwazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mkawakanusha?» Hapo wale wakanushaji walikubali hilo na wasema, «Ndio, wametujia.» Na washika hazina wa Jahanamu wajiepushe na wao na waseme, «Sisi hatutawaombea wala kuingilia kati kuhusu nyinyi. Ombeni nyinyi wenyewe, lakini dua hiyo haitafalia kitu, kwa kuwa nyinyi ni makafiri, na hayawi maombi ya makafiri isipokuwa ni yenye kupotea, hayakubaliwi wala hayaitikiwi.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس