يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهَاۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ
Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enye ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, Mtume wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiulize mambo ya Dini ambayo hamkuamrishwa chochote kuhusu hayo, kama kuuliza kuhusu mambo ambayo hayajatukia au yale ambayo yatapelekea mikazo ya Sheria ambayo lau mlikalifishwa nayo yangalikuwa ni magumu kwenu, na lau mliyauliza wakati wa uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, wakati Qur’ani inateremka, mungalielezewa, na pengine mkakalifishwa nayo na mkalemewa nayo. Hayo Mwenyezi Mungu Ameyaacha ili kuwapumzisha waja Wake nayo. Na Mwenyezi Mungu ni Msamehefu sana kwa waja wake wanapotubia, ni Mpole sana kwao, Hawaadhibu wakirudi Kwake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس