لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ ثَالِثُ ثَلَٰثَةٖۘ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّآ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ وَإِن لَّمۡ يَنتَهُواْ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika wamekufuru Wanaswara waliosema, «Mwenyezi Mungu ni mkusanyiko wa vitu vitatu: Baba, Mwana na Roho mtakatifu.» Kwani Wanaswara hawa hawakujua kwamba watu hawana isipokuwa muabudiwa Mmoja, Hakuzaa wala Hakuzaliwa? Na iwapo wenye kusema maneno haya hawatakoma na uzushi wao na urongo wao, hakika itawapata wao adhabu iliyo kali iumizayo kwa sababu ya kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس