وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّـٰتٖ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡهَٰرٗا
Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Atayaongeza mali yenu na pia watototo wenu, Atawafanya muwe na mabustani ya nyinyi kuneemeka kwa matunda yake na uzuri wake, na Atawajaalia nyinyi muwe na mito ambayo mtaitumia kwa kuipatia maji mimea yenu na pia wanyama wenu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس