Sura Ad-Duha kwa Kiswahili
Ad-Dhuhah · سورة الضحى · Aya: 11 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
وَٱلضُّحَىٰ
Ad-Dhuhah
Naapa kwa mchana! -
2
وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ
Na kwa usiku unapo tanda! -
3
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. -
4
وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرࣱ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. -
5
وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. -
6
أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمࣰا فَـَٔاوَىٰ
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? -
7
وَوَجَدَكَ ضَآلࣰّا فَهَدَىٰ
Na akakukuta umepotea akakuongoa? -
8
وَوَجَدَكَ عَآئِلࣰا فَأَغۡنَىٰ
Akakukuta mhitaji akakutosheleza? -
9
فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ
Basi yatima usimwonee! -
10
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! -
11
وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.