Sura Al-Lail kwa Kiswahili
سورة الليل · Aya: 21 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ
Al-Lail
Naapa kwa usiku unapo funika! -
2
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
Na mchana unapo dhihiri! -
3
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Na kwa Aliye umba dume na jike! -
4
إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. -
5
فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ
Ama mwenye kutoa na akamchamngu, -
6
وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
Na akaliwafiki lilio jema, -
7
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ
Tutamsahilishia yawe mepesi. -
8
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake, -
9
وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
Na akakanusha lilio jema, -
10
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡعُسۡرَىٰ
Tutamsahilishia yawe mazito! -
11
وَمَا يُغۡنِي عَنۡهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? -
12
إِنَّ عَلَيۡنَا لَلۡهُدَىٰ
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. -
13
وَإِنَّ لَنَا لَلۡأٓخِرَةَ وَٱلۡأُولَىٰ
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. -
14
فَأَنذَرۡتُكُمۡ نَارࣰا تَلَظَّىٰ
Basi nakuonyeni na Moto unao waka! -
15
لَا يَصۡلَىٰهَآ إِلَّا ٱلۡأَشۡقَى
Hatauingia ila mwovu kabisa! -
16
ٱلَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Anaye kadhibisha na kupa mgongo. -
17
وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلۡأَتۡقَى
Na mchamngu ataepushwa nao, -
18
ٱلَّذِي يُؤۡتِي مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. -
19
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعۡمَةࣲ تُجۡزَىٰٓ
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. -
20
إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. -
21
وَلَسَوۡفَ يَرۡضَىٰ
Naye atakuja ridhika!