Sura Ash-Shams kwa Kiswahili
As-Shams · سورة الشمس · Aya: 15 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا
As-Shams
Naapa kwa jua na mwangaza wake! -
2
وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا
Na kwa mwezi unapo lifuatia! -
3
وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا
Na kwa mchana unapo lidhihirisha! -
4
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا
Na kwa usiku unapo lifunika! -
5
وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! -
6
وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! -
7
وَنَفۡسࣲ وَمَا سَوَّىٰهَا
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! -
8
فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, -
9
قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا
Hakika amefanikiwa aliye itakasa, -
10
وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا
Na hakika amekhasiri aliye iviza. -
11
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, -
12
إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا
Alipo simama mwovu wao mkubwa, -
13
فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. -
14
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. -
15
وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا
Wala Yeye haogopi matokeo yake.