Sura Al-Balad kwa Kiswahili
سورة البلد · Aya: 20 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Al-Balad
Naapa kwa Mji huu! -
2
وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Nawe unaukaa Mji huu. -
3
وَوَالِدࣲ وَمَا وَلَدَ
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. -
4
لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ
Hakika tumemuumba mtu katika taabu. -
5
أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدࣱ
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? -
6
يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالࣰا لُّبَدًا
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. -
7
أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? -
8
أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ
Kwani hatukumpa macho mawili? -
9
وَلِسَانࣰا وَشَفَتَيۡنِ
Na ulimi, na midomo miwili? -
10
وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ
Na tukambainishia zote njia mbili? -
11
فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. -
12
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ
Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? -
13
فَكُّ رَقَبَةٍ
Kumkomboa mtumwa; -
14
أَوۡ إِطۡعَٰمࣱ فِي يَوۡمࣲ ذِي مَسۡغَبَةࣲ
Au kumlisha siku ya njaa -
15
يَتِيمࣰا ذَا مَقۡرَبَةٍ
Yatima aliye jamaa, -
16
أَوۡ مِسۡكِينࣰا ذَا مَتۡرَبَةࣲ
Au masikini aliye vumbini. -
17
ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. -
18
أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. -
19
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. -
20
عَلَيۡهِمۡ نَارࣱ مُّؤۡصَدَةُۢ
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.