۞شَرَعَ لَكُم مِّنَ ٱلدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِۦ نُوحٗا وَٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَمَا وَصَّيۡنَا بِهِۦٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰٓۖ أَنۡ أَقِيمُواْ ٱلدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُواْ فِيهِۚ كَبُرَ عَلَى ٱلۡمُشۡرِكِينَ مَا تَدۡعُوهُمۡ إِلَيۡهِۚ ٱللَّهُ يَجۡتَبِيٓ إِلَيۡهِ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِيٓ إِلَيۡهِ مَن يُنِيبُ
Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Amewawekea nyinyi, enyi watu, Sheria ya Dini tuliyokuletea kwa njia ya wahyi, ewe Mtume, nayo ni Uislamu, na ile Aliyomuusia Nūḥ aifuate kivitendo na aifikishe kwa watu, na ile aliyowausia Ibrāhīm, Mūsā na Īsā (Watano hawa ndio Ulū al- 'azm [wenye hima] miongoni mwa Mitume kulingana na kauli iliyo mashuhuri) kwamba msimamishe Dini kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kumtii na kumuabudu Yeye na sio mwingine, na msitafautiane katika Dini ambayo nimewaamrisha muifuate. Ni kubwa mno juu ya washirikina lile mnalowalingania la kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada. Mwenyezi Mungu Anamchagua Anayemtaka miongoni mwa viumbe Vyake awe ni mwenye kumpwekesha na Anamuongoza yule anayerejea Kwake afanye matendo ya utiifu Kwake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس