وَإِذَا سَمِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعۡيُنَهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ مِمَّا عَرَفُواْ مِنَ ٱلۡحَقِّۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
NA WANAPO SIKIA yaliyo teremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanachururika machozi kwa sababu ya Haki waliyo itambua. Wanasema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanao shuhudia.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na miongoni mwa yale yanayoonyesha mapenzi yao kwa Waislamu ni kuwa kundi katika wao (nao ni tume ya watu wa Habashah walipoisikia Qur’ani) yalibubujika machozi macho yao wakawa na yakini kuwa hiyo ni haki iliyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wakamuamini Mwenyezi Mungu, wakamfuata Mtume Wake na wakanyenyekea kwa Mwenyezi Mungu wakimuomba awatukuze kwa heshima ya kushirikiana na umati wa Muhammad, amani imshukie, katika kuwatolea ushahidi umma wengine Siku ya Kiyama.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس